GET /api/v0.1/hansard/entries/362123/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362123,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362123/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, vile vile, ningependa kusema kwamba tulizingatie sana suala hili. Nikitafakari, mimi mwenyewe niliinuka na kufikia mahali nilipo sasa kwa sababu wazazi wangu walikuwa wavuvi. Hata hivyo, maskitiko makubwa ni kwamba, babangu asipoenda kuvua samaki leo, nyumbani hatuwezi kuwa na chakula. Hiyo ni kwa sababu jana hakuwa na mahali pa kuwahifadhi samaki wake. Mpaka sasa, hakuna mahali pa kuwahifadhi samaki ili kesho yake upate kuwauza. Unapovua na kuweza kupata samaki wengi, inabidi utumie wale ambao unaweza kutumia na uwatupe wengine kwa sababu ya ukosefu wa mahali pa kuwahifadhi."
}