GET /api/v0.1/hansard/entries/362124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362124,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362124/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, nawaomba ndugu zangu wote ambao wako hapa tuliangazie suala hili vizuri ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu wavuvi waweze kuendesha maisha yao. Tuhakikishe kwamba katika sehemu zote ambako shughuli za uvuvi hutekelezwa kutakuwa na vifaa vya kuhifadhia samaki. Kwa mfano, Faza, Kizingitini na Kiunga ni sehemu ambazo zinafaa kuwa na vifaa vya kuhifadhia samaki ndiyo wavuvi wanapokwenda kuvua wajue watawahifadhi samaki wao wapi. Hali ilivyo hivi sasa ni kwamba, mtu anaenda baharini na Mwenyezi Mungu anambariki anapata samaki wengi; lakini hajui kwa kuwahifadhi samaki hao. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwetu sisi"
}