GET /api/v0.1/hansard/entries/362139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362139,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362139/?format=api",
"text_counter": 335,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ababu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Mhe. Naib Spika wa Muda, ningependa kuunga mkono Hoja ya Mhe. (Ms.) Odhiambo-Mabona ya kubadilisha kidogo tu Hoja ya Mhe. Ngâongo. Nitaanza kwanza kwa kuwakumbusha Wabunge na Wakenya wote kwamba uvuvi unachangia pakubwa katika uchumi wa Taifa hili. Ninaposema hivyo, nasema mchango kwenye viwango mbalimbali. Kuna viwango vya wale ambao wanategea uvuvi moja kwa moja kama wavuvi katika pembe zote za taifa letu kutoka Bahari ya Hindi hadi Ziwa Victoria. Pia, samaki hupatikana katika mito mbalimbali kama vile Mto Tana, Mto Nzoia na mito mingine kwenye taifa letu. Pia, hupatikana katika maziwa mengine kama vile Ziwa Turkana na Ziwa Naivasha. Kuna Wakenya wengi ambao wanaishi katika maeneo haya ambao tegemeo lao kuu katika maisha yao ni uvuvi. Vile vile, kuna Wakenya wengine ambao wanategemea uvuvi katika hali zingine. Kuna wafanya biashara na wachuuzi wa samaki katika sehemu mbalimbali za taifa letu wanaofanya biashara katika viwanda ambavyo biashara yao ni samaki katika sehemu mbalimbali za taifa hili, iwe ni Kisumu, Thika au Mombasa. Kuna wale ambao wako kwenye biashara ya kuuza samaki kwenye mataifa ya nje hasa katika Muungano wa Mataifa ya Ulaya (European Union). Kwa hivyo, uvuvi ni msingi mkubwa kwenye uchumi wetu kama taifa. Lakini kidogo, kumekuwa na upungufu mkubwa kutoka kwa Serikali tunapozungumzia misaada kwenye sekta ya uvuvi. Tayari, wenzangu waliozungumza hapo mbeleni wametaja msaada mkubwa ambao wakulima wa kawaida wamepata kutoka kwa Serikali. Tumeshuhudia hapo mbeleni Serikali ikifutilia mbali madeni makubwa, mabilioni ya fedha, katika sekta kama vile kahawa, mpunga, sukari lakini hatujashuhudia hatua yoyote kama hii kwenye"
}