GET /api/v0.1/hansard/entries/362142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362142,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362142/?format=api",
"text_counter": 338,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "sekta ya uvuvi, ilihali tunajua, kwa mfano, kuna mashirika ya wavuvi katika sehemu nyingi za taifa hili likiwemo eneo Bunge la Budalangi nilalowakilisha. Hayo ni mashirika ambayo yana malimbukizi makubwa ya madeni kwa sababu ya hali ngumu inayowakumba wafanya biashara. Lakini hatujawahi kushuhudia hata siku moja hatua moja ya Serikali ya kutoa nafuu yoyote kwa mashirika ya wavuvi kupitia kufutiliwa mbali kwa madeni ama kutoa msaada wowote wa dharura. Kwa hivyo, Hoja hii ni ya kutukumbusha kwamba hii ni sekta moja ya uchumi ambayo, ingawa inachangia pakubwa kukuza uchumi wetu, Serikali haijadhihirisha kwa njia yoyote nia ya kuwekeza na kuikuza sekta hii, ilhali sekta hii inaendelea kutuletea fedha nyingi za kigeni. Kiwango kikubwa cha samaki wanaotoka kwenye sehemu ambazo nimetaja kama vile Ziwa Victoria, Bahari Hindi, Ziwa Naivasha na Ziwa Turkana huuzwa kwenye mataifa ya nje na huletea taifa hili letu kiasi kikubwa cha pesa za kigeni ambazo ni mchango mkubwa kwa uchumi wetu. Kwa hivyo, ni changamoto kwa Serikali hii kudhihirisha kwamba ina nia ya kukuza uchumi na kuwekeza katika sekta zote. Tunengependa kuona hatua maalum zikichukuliwa na Serikali hii. Kwa mfano, tungependa kuona utafiti kwenye sekta hii---"
}