GET /api/v0.1/hansard/entries/362146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362146,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362146/?format=api",
"text_counter": 342,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ababu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mhe. (Ms.) Khamisi bado ni mgeni kwenye Bunge hili. Kwa hivyo, tunaweza kuelewa kidogo. Nilikuwa nazungumzia swala la utafiti. Serikali inatumia kiwango kubwa zaidi cha fedha kufanya utafiti katika sekta ya ukulima, kwa mfano, kupitia mashirika kama vile KARI na mengineo. Lakini hatujaona utafiti wowote ukifanyika ama matunda ya utafiti wowote katika sekta hii ya uvuvi. Mhe. (Ms.) Odhiambo-Mabona ametaja hatua ya kipindi ambacho wavuvi huzuiwa kufanya biashara yao - closed season. Kipindi hicho kifikapo, wavuvi wote wanazuiwa kufika katika maeneo ya uvuvi. Kwa muda huo wote, inamaanisha kwamba wavuvi wote hawako kwenye kazi yoyote. Kumbuka wavuvi hao wanategemea uvuvi kama chakula chao na kuwaelimisha watoto wao. Katika hali zote za maisha yao, wao hutegemea uvuvi huo na kwa hivyo, ukiwafungia kazi yao kwa muda wa miezi minne--- Ikiwa sisi Wabunge tutaambiwa hatutafanya kazi hapa kwa muda wa mieze minne na hakutakuwa na malipo yoyote; hakuna mshahara na hakuna marupurupu kwa muda ambao tunaketi kwenye Bunge hili ama kwa Kamati, naamini hakuna Mbunge yeyote atakubali hatua kama hiyo. Sasa wewe tafakari ujiulize: Mvuvi kwenye kijiji cha Mbita, Budalangi ama Turkana afungiwe njia yake ya pekee ya kujimudu kwa muda wa miezi minne mfululizo, atafanya nini? Jiulize: Mvuvi huyo atajimudu namna gani? Tafakari hayo kwenye Bunge hili la kifahari. Huyo mvuvi atajimudu namna gani? Na wakati wa kipindi hicho cha kufunga uvuvi, ni muda ambao huwa ni mgumu sana kwa wavuvi na familia zao."
}