GET /api/v0.1/hansard/entries/362149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362149,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362149/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Naamini Serikali ina uwezo wa kufanya utafiti na kuongeza idadi ya samaki kwenye maeneo hayo - yaani re-stocking . Hatujawahi kushuhudia wakati wowote kwa muda mrefu sana Serikali ikichukua hatua ya kufanya utafiti na kuongeza idadi ya samaki kwenye maziwa yetu kupitia mpango huo wa re-stocking . Kwa nini? Ni hatua ambayo inachukuliwa katika mataifa mengi ulimwenguni ambayo yanategemea uvuvi. Huu ni uzembe kwa upande wa Serikali. Serikali inataka kuzembea kazi na kukimbilia hatua ya Rais ya kufunga uvuvi, ilhali, hatua inayofaa ni mpango huo wa kuongeza idadi ya samaki kwenye maziwa na mito yetu kupitia mpango huo wa re-stocking. Ni changamoto kwa Serikali hii ya digitali. Tungependa kuona samaki wakiongezwa kwenye maziwa yetu kupitia njia ya digitali na Serikali hii ya digitali."
}