GET /api/v0.1/hansard/entries/362164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362164,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362164/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, Serikali pia inachangia katika uzembezi wa sekta hii ya uvuvi kuhusiana na barabara. Barabara zina matatizo haswa katika wakati huu wa mvua ilionyesha sana. Utakuta sasa hivi barabara ambayo inasaidia Kenya na Tanzania imekatika. Mpaka sasa hivi, hakuna mikakati ambao imewekwa kisawasawa ya kuhakikisha kwamba barabara hiyo imetengenezwa. Vile vile, katika ramani ya Kenya, kuna barabara mbili ambazo ni kubwa zinazochangia katika sekta ya utalii. Kwanzia Kanana kwenda Shimoni, ni barabara ambao ni ya kilomita 15. Pia kwenye ramani ya Kenya, barabara hiyo inatakikana iwe na lami. Vile vile, nikizungumzia barabara ya kutoka Lunga Lunga kuingia Vanga, inachangia uvuvi na sekta ya utalii. Barabara hiyo iko kwenye ramani ya barabara ambazo zinatakikana kuwekwa lami. Lakini haina lami. Mara nyingi, imetumiwa na wanasiasa kuomba kura. Wanasema: “Mkinichagua, katika kipindi cha miaka mitano, nitahakikisha kwamba, kwa vile barabara hii iko kwenye ramani, itawekwa lami. Yaani, nitahakikisha kama Mbunge wenu kwamba nitawawekea barabara ya lami.” Kwa hivyo, kwa vile mimi nilitumia kigezo hicho kama njia ya kupata kura, naomba Serikali inisaidie katika jukumu hilo. Serikali inijengee hizo barabara mbili ili niweze kurudi Bunge baada ya miaka mitano."
}