GET /api/v0.1/hansard/entries/362169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362169/?format=api",
"text_counter": 365,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Vile vile, moja kati ya juhudi za Serikali ya Jubilee ni kuhakikisha kwamba vijana wamepata kazi. Lakini, nasikitika sana kwa mashiriki makubwa ya Serikali. Vijana wengi wanafanya bidii kumaliza masomo katika vyuo vikuu ili waajiriwe kazi katika mashiriki ambayo yanalipa vizuri. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba Shirika la Ushuru la Kenya liliajiri vijana mwaka uliopita. Lakini hakuna hata mmoja ambaye aliajiriwa kutoka katika eneo langu la Bunge. Kupitia kwako, Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningeomba KRA itoe majina yote ya wale ambao waliajiriwa kazi mwaka jana ili tuweze kuyachambua na kujua ni mikakati gani iliyotumika kuwaajiri kazi."
}