GET /api/v0.1/hansard/entries/362171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362171/?format=api",
"text_counter": 367,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuunga mkono Hoja hii, ambayo imeletwa na hon. Ngâongo. Pia, nataka kuunga mkono mabadiliko ambayo yameletwa na hon. (Ms.) Odhiambo-Mabona. Tunajua ya kwamba katika sehemu nyingi katika Jamhuri yetu ya Kenya, watu wengi wanategemea kilimo cha samaki. Hivyo basi, iwapo tutawazuia kupata ajira yao au kupata pesa ya kuwakidhi katika maisha yao, itakuwa ni jambo la kutatanisha. Kwa hivyo, muda wa mwezi mmoja utakuwa muda mzuri wa mtu kuweza kujisatiti na pengine kujipanga vizuri katika hali yake ya maisha. Nataka kuchangia jambo fulani katika kilimo cha samaki. Kwanza kabisa, hazina hiyo itakapoundwa, wataweza kupata pesa za kuwasaidia pengine kwa mambo ya vifaa vya kuwekea samaki wasioze, ama vifaa vya uvuvi. Wavuvi wetu wamekuwa wakitumia madao ya zamani na ngalawa. Hivyo basi, hawawezi kufika mbali. Pia, hawawezi kupata samaki kwa njia inayofaa. Fedha hizo pia zitaweza kuwapatia mafunzo wavuvi wetu wadogo ili waweze kujua mbinu za kisasa ambazo zitawafanya waweze kuwa na kilimo bora cha samaki. Jambo la pili, fedha hizo pia zitaweza kuwafunza wavuvi juu ya mazingira. Ni lazima mazingira yawe bora kwa samaki wetu. Kwa hivyo, ni lazima sera na kanuni ambazo zimewekwa juu ya uvuvi zifuatwe na Wakenya na wasiokuwa Wakenya ambao wameingia katika kilimo cha samaki. Nasema hivyo kwa sababu kuna watu kutoka nchi za nje ambao wamekuja kufanya uvuvi katika bahari na maziwa zetu. Wanatumia majerifa ama trawlers ambazo zinavunja zile nyumba za samaki na yule mvuvi wa hali ya chini anakosa samaki. Hawezi kwenda ndani ya bahari au deep sea . Jambo hilo linaleta matatizo mengi sana. Wanaofaidika ni wale ambao wanatoka nje kuliko wavuvi wetu ambao ni wadogo. Kwa hivyo, inahitajika Kenya Ports Authority ilinde sehemu zetu kuhusiana na wavuvi ambao wanafanya uvuvi wa haramu. Pia, Kenya Navy inatakikana kufanya kazi ya kuangalia na kuona ikiwa wavuvi hao wanafuata kanuni zinazohitajika. Sisi tuna Muungano wa Afrika Mashariki ambao unajumuisha Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi. Lakini wavuvi wetu wanapofika karibu na sehemu ya Tanzania, wanashikwa. Mambo kama hayo yametokea katika maeneo Bunge ya Msambweni na Lunga Lunga. Wavuvi wetu wengi wamekuwa wakilala katika seli wakati wanatumia raslimali ambazo ziko katika nchi yetu ya Kenya. Jambo lingine ni kwamba tumekuwa na miradi ya samaki wa vidimbwi. Pesa nyingi za Wakenya zimetumiwa kuchimba vidimbwi katika sehemu nyingi. Masikitiko yangu ni kwamba vidimbwi vingi sasa vimekauka na havina samaki. Serikali inafaa"
}