GET /api/v0.1/hansard/entries/362174/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362174,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362174/?format=api",
"text_counter": 370,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwamba ni lazima kuwe na hazina ama pesa ambazo zitaamsha vidimbwi hivyo kwa sababu hatuwezi kutumia malioni ambayo Wakenya wanatoa kupitia ushuru kutengeneza vidimbwi kiholela na ambavyo havitupatii faida katika nchi yetu. Kuna vile ambavyo vimefanywa vizuri na tunakubali. Lakini vingi havikufanywa katika njia nzuri. Kwa hivyo, ni lazima swala hili tulirudie kwa undani sana ili tuweze kulirekebisha. Jambo lingine ni lile kwa Kiingereza tunaliita âfish landingâ. Ni sehemu ambazo wavuvi wanaweza kuweka samaki wao. Sehemu hizo zimechukuliwa kiholela. Ukitembea katika sehemu ya Nyanza, Pwani na Bonde la Ufa ambapo tunapata kilimo cha samaki, utapata kuwa hakuna sehemu kama hizo. Wizara ya Ardhi ni lazima ifungue macho yake na iangalie ya kwamba wavuvi wetu wana sehemu ambazo wanaweza kuendeleza kilimo cha samaki. Tunataka kuboresha kila kaunti katika Jamhuri yetu ya Kenya, lakini pahali ambapo rasilmali inapatikana panahitajika kuwa na kiwanda ili kukuza na kuboresha raslimali hiyo ili uchumi wetu wa Kenya uendelee. Serikali ya Jubilee imesema kwamba itaendeleza uchumi wetu uwe â double"
}