GET /api/v0.1/hansard/entries/362176/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362176,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362176/?format=api",
"text_counter": 372,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "â. Hata kama ni â by double digits â au kuongeza mara dufu, ni lazima tuangalie kilimo hiki kwa njia ya undani kabisa. Lazima tutengeneza viwanda kama kile cha Thika. Kile kiwanda ambacho kiko pale Thika, tunakikubali na tunashukuru Serikali kwa kukijenga. Lakini, tukiwa na kiwanda kama hicho katika Nyanza au Pwani, ambapo raslimali hiyo ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia iko kwa wingi, ajira kwa vijana, kama inavyosema Serikali ya Jubilee, itapatikana. Pia, tutaweza kuboresha kilimo kwa sababu samaki si samaki peke yake. Samaki kama omena anaweza kusiagwa ikachanganywa na mawele na wimbi na ikawa chakula kizuri kwa watoto wetu wachanga na hata wazee ambao nguvu zao zimepungua. Lakini ikiwa kilimo cha samaki kitachukuliwa tu ni kukaanga au kuchoma, hatutasaidika. Ni lazima tujue samaki anaweza kuleta bidhaa nyingi sana. Kuna keki ambazo zinatengenezwa kutoka kwa samaki. Mifupa ya samaki pia huvunjwa na kutengenezwa dawa ambazo zinatibu maradhi mengi sana. Hilo ni jambo nzuri sana. Tungependa kupata soko la samaki wetu. Hakuna samaki mwenye radha kama anayetoka Nyanza ama Pwani. Ukweli na tuuseme! Leo hii, Wakenya wanaletewa samaki kutoka nje. Wametiwa ndani ya mikebe ambao imekaa katika mafiriji kwa miaka mingi sana. Sisi tuko na samaki walio freshi ambao hata ukifika pale Kisumu, unajua kweli unakula samaki na unasikia kweli ni ladha ya samaki unayokula. Wakenya ni lazima tuamke na tujue hiki ni kilimo cha kujenga nchi yetu na kuongeza uchumi ambao Serikali ya Jubilee iliahidi. Mwisho, kuna mashirika ya uvuvi. Hatukiangazii kilimo cha samaki na fedha ambazo zinafika kule hatuzichunguzi. Zinapotea! Kuna ufisadi wa hali ya juu. Tunataka kuboresha zile Beach Management Units (BMUs) ambazo zinasimamia wavuvi. Hicho ni kilimo bora ambacho kinaweza kutulisha sisi Wakenya na kutupatia ajira kwa vijana wetu. Kwa hivyo, ni lazima tulichukulie jambo hili kwa mwafaka. Akina mama wanaokaanga samaki wanakosa hata mahali pa kuweka samaki wao. Wanatakiwa pia wapate afya bora na sindano ambazo zitawawezesha kujikinga kutokana na moto mkubwa ambao wanatumia kukaangia samaki. Hao ni akina mama maskini. Na kwa vile tunasema shabaha yetu ya 2030 ni kuondoa umaskini na kuboresha akina mama, pia hazina hiyo iwasaidie akina mama. Wakati watu wa nje wanakuja kama vile Tiomin na Titanium na kuchimba bahari yetu na kuweka mabohari, wavuvi hawawezi kuvua samaki"
}