GET /api/v0.1/hansard/entries/362331/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362331,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362331/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "majibu ya kutekeleza sheria ya nchi moja; Bunge la Taifa na Bunge la mashinani. Pili, utawala wa Taifa na utawala wa mashinani. Tatu ni Mahakama. Utakapopeleka Bunge upeana 43, nani amekupatia mwongozo kwa sababu Kufungu cha 3 cha Katiba kimetoa mwongozo? Bunge ndilo la kwanza litakalofanya ranking. Naibu Spika, Baraza la Mawaziri limepewa namba sita na sisi ndio tumewapitisha hapa Bunge. Wengine wameshtuka kabisa, wakachanganya mafuta na maji. Sisi ndio tumewakosoa, tukawarekebisha na tukawaambia chukua ofisi. Hawatuandiki kazi! Serem alikuja hapa akaapa kwamba hatateremsha mishahara ya wafanyi kazi kiholela, na huko ndiko anafanya kazi. Naibu Spika, nimesimama kuunga Hoja hii mkono. Waswahili wanasema: Kila nyani ana siku yake. Waliochinja nguruwe wana siku yao. Sisi tuna siku na siku yetu ni siku ya Katiba. Sisi hatutachinja nguruwe. Nataka nisikike vizuri kule nje. Leo ni maswala ya Katiba, Sarah Serem angalie Kifungu 94 (1), (3), Kifungu 3 cha Katiba ya Nchi. Amevunja Sheria kulia, kushoto, kusini, kasikasini na katikati."
}