GET /api/v0.1/hansard/entries/362676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362676,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362676/?format=api",
"text_counter": 484,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ashante sana Naibu Spika. Hata mimi ninaunga mkono Hoja hii kuhusu Bw. Kimemia. Kwa kweli mimi sijui ni watu gani katika Kenya tunataka! Ukiangalia ile kazi Bw. Kimemia amefanya katika nchi hii, nafikiri ni mtu ambaye anastahili kupatiwa kazi hii. Badala ya kuongea mengi, tungepitisha Hoja kwa sababu naona kila mtu hapa ni rafiki ya Bw. Kimemia. Yafaa tuseme kwamba tunajua kazi yake. Kwa kweli ni mtu mwenye roho safi; hata ukiwa na shida, kama sisi ambao tuna shida ya usalama, na umpigie simu saa tisa usiku atachakua. Ukimweleza shida zako, atafanya kile wakenya wanataka. Kwa hivyo, ninaonelea kwamba, badala kukaa hadi saa nne au saa tano tukijadiri Hoja hii kuhusu Bw. Kimemia, kila mtu ni rafiki yake hapa na wengi wanampenda na kazi yake iko sawa. Naona mhe. Ababu anacheka pale; pia kuna rafiki yangu pale anaitwa Midiwo. Ningeomba tuweke sahihi na kumaliza jambo hili. Ninaunga mkono."
}