GET /api/v0.1/hansard/entries/362693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362693,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362693/?format=api",
"text_counter": 501,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Bi. Naibu wa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu ni ya muhimu sana. Nimesikia kuna mtu ambaye aliandikia Bunge barua kuhusu suala la IDPs. Kuhusu suala hili, ningependa kusema kwamba nimeshughulika sana na masuala ya IDPs. Ninathibitisha kwamba kama kuna mtu ambaye aliwasadia sana IDPs, kwa kuwapa makao; ni Bw. Kimemia. Mimi na mkazi wa Nakuru,na ninajua shida tulizokuwa nazo kuhusu IDPs lakini Bw. Kimemia alisaidia sana kwa kusikiliza maoni na hata kwenda kuangalia maslahi ya IDPS walipokuwa wakipewa makao. Kwa hivyo, ninaomba, kwa sababu tumelizungumzia jambo hili kwa kirefu: Sisi sote tuko pamoja. Kwa hivyo, tuchukue fursa hii tuseme tumekubaliana na Kamati ambayo imeleta pendekezo hili Bungeni. Kamati hii imefanya kazi nzuri sana. Kama alivyosema mheshimiwa fulani, tunamuheshimu sana Bw. Kimemia kwa jinsi alivyoweza kutuambia mambo yake yote kumhusu. Ninaiunga mkono Hoja hii. Kwa hivyo, tuipitishe kwa kauli moja ili tushughulikie jambo lingine. Tumeizungumzia Hoja hii kwa masaa mengi sana kwa sababu ya heshima. Kwa hivyo tuipitishe. Bi. Naibu wa Spika, kwa hayo machache, ninakuomba uulize Swali tuipitishe Hoja hii."
}