GET /api/v0.1/hansard/entries/363003/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 363003,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363003/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia hii nafasi. Namshukuru Mhe. Gitari kwa kuleta hii Hoja Bungeni kwa sababu ugonjwa wa saratani umeangamiza watu wengi nchini Kenya. Vile vile ni kwamba watu wengi wanaoishi vijijini, hasa kina mama, wanapata shida sana na ugonjwa wa saratani, na hawawezi kufikia matibabu. Hospitali nyingi za mkoa hazina vifaa kama hivyo na pia hawapati kuhamishwa kwa sababu ya ugonjwa huu. Wakati ambapo tunasherehekea mwaka wa Jubilee, kuna mambo mengi ambayo tumejaribu kupigana nayo hapa Kenya, mojawapo ikiwa ni magonjwa na ugonjwa huu wa saratani umekuwa hatari kubwa. Kwa hivyo, ni lazima Serikali ichukue hatua na kutilia maanani kama itawezekana kuwa na vifaa vya kupima saratani na kuuguza. Zaidi ya hayo ni heri tuwafahamishe watu katika kila kaunti kuhusiana na ugonjwa wa saratani; kina mama wafundishwe jinsi gani wanaweza kujichunguza wenyewe kabla hawajakumbwa na saratani ya matiti. Pia, tuwahamasishe watoto kwa sababu si wazee peke yao wanaopata. Hata akina mama wa makamu na watoto wanapata saratani. Kwa hivyo, itakuwa jambo la maana kama Serikali itaweza kuwa na vifaa katika kila mkoa ama kaunti ili tuweze kuupiga vita ugonjwa huu au kuchunguza. Sana sana nitakuwa nasimamia upande wa kina mama kwa sababu wanapata saratani ya kizazi; wengi wanakosa kupata watoto kwa sababu ya ugonjwa huu. Kwa hivyo, hili litakuwa ni jambo la maana. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}