GET /api/v0.1/hansard/entries/363234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 363234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363234/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika. Kwanza, ninamshukuru Mhe. Wakhungu kwa kuleta Hoja kama hii wakati huu. Niko katika biashara ya kuingiza mali nchini, lakini ninauliza: Serikali ina taasisi za kuchambua na kuangalia hali ya hewa ili kujua ni lini tutapata mvua na ni lini tutakoza mvua? NCPB haileti mbolea ikiwa imechelewa lakini kuna matatizo ndani yake. Haya matatizo ni kwa sababu ya mivumo yao. Ikiwa Serikali itaweza kuipatia habari taasisi kama hii na kuhakikisha kuwa imeleta mbolea wakati ufaao ili wakulima wapate hiyo mbelea mapema, basi hatutakuwa na matatizo kama haya. Kama vile mwenzangu aliyenitangulia amesema, hii ni kwa sababu ya ufisadi ambao umeendelea sana. Iwapo Serikali itaamua kuwa na taasisi ya kusimamia kuleta mbolea peke yake, ningeiomba iweke mikakati kabambe. Nimesikia kuna mbolea na mbegu zinazotolewa kwa wakulima lakini sijasikia hata siku moja wakulima kwenye sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni wakipewa mbegu ama mbolea. Tumekaa kwenye umaskini kwa muda mrefu. Ninaamini kwamba Serikali itasimama kidete kuhakikisha kwamba wakulima katika maeneo yote nchini wamepata usaidizi kwa sababu usaidizi ni mwafaka. Niko na uhakika kwamba wale ambao wanapanda mimea watafaidika. Wakipata usaidizi kama huu, wataweza kuifanya kazi na waongeze mapato yao. Vile vile, ningependa kuiomba Serikali ieleze mikakati iliyoweka kwa sababu bali na mbolea, kuna mambo mengi yanayochangia kuongezeka kwa mazao ya kilimo ili mwananchi aweze kuendeleza maisha yake. Bali na mbolea, kuna matatizo mengine. Kwa mfano, mvua ikinyesha sana, mimea hubebwa na maji. Kuna matatizo ya mimea kuharibiwa na wadudu na matatizo ya kuuza mazao. Hayo yote ni matatizo ambayo Serikali inapaswa kuyashughulikia kwa dhati ndio tupate majibu kamili. Leo tukisema mbolea itakuja, je, madawa ya kunyunyizia mimea yatafika vipi? Je, mbegu zitafika vipi? Hayo yote ni matatizo tuliyonayo. Kwa hivyo, ninaiunga mkono Hoja hii lakini itakapobuniwa taasisi inayopendekezwa, ni lazima tuhakikishe kwamba tumeweka mikakati kabambe itakayowaongoza wale ambao wataifanya kazi hiyo; tusipozingatia matatizo yanayoikumba NCPB, ‘ugonjwa’ wake utairukia bodi ya mbolea. Kwa hivyo, ninaliomba Bunge lihakikishe kwamba mikakati mizuri imewekwa. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}