GET /api/v0.1/hansard/entries/363308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 363308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363308/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii imekuja wakati unaofaa lakini ni lazima kwanza tuangalie chanzo cha matatizo haya. Alipokuwa Waziri wa Kilimo Makamu wa Rais William Ruto, wakulima katika eneo la Pwani walivuna chakula kingi mpaka wakakosa mahali pa kukihifadhi na kikaoza. Kuna shida katika Wizara ya Kilimo. Tunaomba Waziri wa Kilimo wa sasa aige mfano wa Mheshimiwa Ruto. Tunaomba asikae ndani ya ofisi bali aende mashambani akajionee na awasikize wananchi. Halmashauri ya nafaka nchini imejitweka majukumu yakuleta mbolea, ambayo si majukumu yake. Kama halmashauri hiyo imeshindwa kutuletea mbegu, italeta mbolea? Tumeipitisha Katiba ambayo imeanzisha serikali za majimbo. Sielewi ni kwa nini mpangilio wa ugavi wa mbegu ama mbolea umebaki katika Serikali Kuu. Inafaa kila kaunti inayofanya shughuli za kilimo ipelekewe pesa inunue mbolea na kuwapatia wakulima. Mamlaka ya kununua mbegu yatakapopewa kaunti na taasisi iliyopendekezwa kuundwa, bodi ndogo katika kaunti zitapatiwa hayo mamlaka na tutaweza kupata mbegu na mbolea kwa wakati unaofaa. Wakati huo itakuwa rahasi kuwatambua wale ambao watakuwa wanazembea katika kazi zao, kinyume na hali ilivyo sasa, ambapo uzembe uko katika Serikali Kuu. Wakenya wanalia kwa sababu mbegu na mbolea haziwafikii kwa wakati unaofaa. Ninakumbuka kwamba katika miaka ya 90, kule kwetu Pwani kuliletwa mbegu iliyoitwa “Coast Composite”. Mbegu hiyo ilizaa ajabu lakini kulipoonekana kwamba Wapwani walianza kupata chakula, mbegu hiyo iliangamizwa. Sasa tunaletewa mbegu ndani ya mifuko. Tunaambiwa ndiyo mbegu inayofaa lakini tukipanda mahindi yanazaa yakiwa futi moja. Tutapata vipi chakula sisi Wapwani? Bi. Naibu Spika wa Muda, wakati umefika wa haki kutendeka kupitia kwa majimbo yetu. Nina imani kwamba Serikali hii itaweza kutilia maanani kwamba bila ya chakula hatuwezi kufika popote. Kilimo ni njia moja ya kuleta ajira. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea ni njia moja ya kuleta ajira. Nchi kama Israel inaweza kutengeneza mbolea yake. Unapoingia Mombasa na sehemu nyingine za Nairobi, unashindwa hata pa kupitia. Kunanuka uvundo. Uchafu umeenea kila mahali licha ya kwamba uchafu huo unaweza kugeuzwa na kufanywa mbolea. Tunaomba shirika lililopendekezwa liundwe lihakikishe kwamba katika kila eneo kutakuwa na kiwanda cha kutengeneza mbolea. Tukifanya hivyo, tutaweza kuisafisha miji yetu na kuwa na mazingira masafi. Tutakuwa tumeua ndege kumi kwa jiwe moja. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}