GET /api/v0.1/hansard/entries/363512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 363512,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363512/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bw. Spika, Kipengele cha 152(2) cha Katiba ya Kenya kimetoa mamlaka ya kuteuliwa kwa Mawaziri. Kipengele cha 204(4) cha sheria ya Bunge kinakubalia ile kamati inayoamua iwapo aliyependekezwa na Rais anafaa kuwa Waziri au hafai. Mimi ninafuraha tofauti na wengine. Furaha yangu inatokana na mambo mawili. Nimefurahi, kama mfugaji. Kwa upande wa ufugaji, niko na ole Lenku. Pili, nimefurahi kama Mpwani. Kama Mpwani, niko na mhe. Kazungu Kambi. Kwa nini nimefurahi? Ni watu wachache kutoka Mkoa wa Pwani waliosimama kidete kuiunga mkono Serikali ya Jubilee. Mimi, nikiwa miongoni mwa wale wachache, sikusikitika wala kujuta kwa kumchagua Uhuru Kenyatta kama Rais wangu. Matunda ndio haya."
}