GET /api/v0.1/hansard/entries/363518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 363518,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363518/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Kuna mzozo unaotokota hivi sasa. Serikali imetoa amri operesheni ifanywe. Operesheni hiyo inafanywa katika Taita Ranches. Ng’ombe 80,000 wa wafugaji wako katika Taita Ranches. Kwa bei ya soko leo, thamani ya ng’ombe hao ni kati ya Ksh3.5 billion na Kshs4 billion, lakini Serikali iko tayari kwenda huko na helikopta na kuwafukuza ng’ombe hao. Bw. Spika, wafugaji walienda mahakani wakapewa court order inayoiamrisha Serikali kusitisha operesheni hiyo, lakini Serikali imekataa kutii amri ya mahakama. Tulianzia kwa ofisi ya Katibu wa Kudumu, tukateremka chini lakini amri ya mahakama ilikataliwa. Je, wafugaji wanadhulimiwa kwa sababu wao ni Wasomali? Wanadhulumiwa kwa sababu wao ni wafugaji? Kwa nini waandishi wa vyombo vya habari hawayaangazii mambo haya? Katika Kenya ya leo, mahakama inatoa amri Serikali isitishe operesheni ya kuwafurusha mifugo kutoka mbuga za wanyama pori, lakini hakuna mtu anayesikia kwa"
}