GET /api/v0.1/hansard/entries/363768/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 363768,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/363768/?format=api",
"text_counter": 358,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, mbali na hayo, tutajaribu kuhimiza Serikali kuja na mipango kama ya kuangalia zile hospitali ambazo ziko sasa hivi. Kwale ama Msambweni tuna referral hospital moja ambayo inaitwa Msambweni Referral Hospital. Lakini hamna madaktari. Daktari ni mmoja, alale usiku halafu mchana aje kazini. Kukiwa na tatizo lolote la utabibu wa haraka, wanaofanya kazi ni wasaidizi. Kwa hivyo, naomba Serikali pia ione tumepata vifaa sawasawa katika hospitali zetu. Tutaweza kupambana na magonjwa madog madogo kisambamba. Tutaweza kutibu magonjwa makubwa na madogo. Tutayatibu kwa haraka kwa sababu wananchi wanapoteza maisha yao haraka. Ikiwa Serikali itaingilia swala hili, itakuwa ni wazo mwafaka."
}