GET /api/v0.1/hansard/entries/364460/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364460,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364460/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Bw. Spika, kwanza, ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu, sisi, kama wanakamati wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, tuliketi pamoja tukakubaliana juu ya Ripoti hii. Hakuna mwanakamati hata mmoja aliyepinga masuala ambayo Mwenyekiti wetu ameyaangazia. Kwa hivyo, ninawasihi wanasiasa wasilete siasa kwa ugavi wa mali humu nchini, na haswa kuhusu masuala ya Bajeti. Kama kuna jambo ambalo walitaka kulizungumzia, wangekuja kwenye ile mikutano iliyoandaliwa washikadau kule mashinani. Wangezungumzia mambo hayo wakati huo. Kwa hivyo, haifai mtu yeyote kusema kwamba hatukufanya vile walivyotushauri tufanye."
}