GET /api/v0.1/hansard/entries/364465/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364465,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364465/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, hata Mamlaka ya Mpito haijui hela tunazotengea serikali za kaunti zitatumiwa namna gani. Mamlaka hiyo haijui bei za vitu. Haijulikani ni kitu gani kinatakiwa kufanywa. Kwa hivyo, wametushauri tuwapatie Magavana hela walipe mishahara ndiyo waanze kujiandaa kwa miradi watakayofanya. Mwaka ujao, tutaanza kuangalia iwapo kumekuwa na makosa ama la. Mwenyekiti wetu alijaribu sana kutusihi; alituuliza kama ingewezekana kwa serikali za kaunti kuongezewa pesa. Walisema hawakuwa na pesa ambazo wangetumia kwa maendeleo. Kwa ujasiri wa Mwenyekiti wetu, tulikubaliana kuwa hivi karibuni tumwite Waziri wa Fedha, magavana wote and hii Kamati ya Bajeti tuzungumzie vile mwaka ujao pesa zitagawanywa kwa serikali za kaunti."
}