GET /api/v0.1/hansard/entries/364800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 364800,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364800/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Shukrani, Bw. Naibu Spika wa Muda. Masikitiko makubwa ni kwamba utapata sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya hazipati huduma za afya vile inavyopaswa. Nikizungumzia eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, licha ya kwamba kupatikana madaktari ni vigumu, hata hospitali zenyewe, ama hata zahanati zenyewe, hazina madawa. Watu huenda na kurudi; hata ingawa hufika huko akiwa mgonjwa anaambiwa kwamba dawa hakuna. Kwa hiyo, mara kwa mara watu wamekuwa wakisumbuka au kuteseka. Hata huduma za X-ray hazipatikani. Leo Serikali imesema kwamba wanawake watajifungua bure, lakini utapata hakuna sehemu ya akina mama ama akina dada zetu ya kujifungulia katika eneo la Lamu Mashariki. Utapata kwamba madaktari ama wahudumu ambao wako pengine ni mmoja katika zahanati; ama pengine utapata siku ya kazi mtu anapaswa awepo kazini, lakini wagonjwa wanaenda hospitalini na kupata kwamba hata yule mmoja ambaye anapaswa awe pale hayupo. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukweli ni kwamba sisi tunazungumza mambo haya lakini maeneo Bunge mengi yana matatizo hasa mashinani. Mimi naunga mkono Hoja hii na bali na kuiunga mkono, ningependa kupendekeza kwamba yote yatakayopitishwa katika Bunge hili kuhakikisha kwamba sio kwamba tumeyazungumza hapa Bungeni kwa sababu ya kuyazungumza, ama kwa sababu ni Hoja imeletwa--- Inafaa tuhakikishe kwamba mambo haya yameweza kuwasaidia ndugu zetu, ama jamii ambazo zimeweza kuteseka kwa muda mrefu. Hivi sasa wanahitaji kupata zile huduma ambazo Serikali hii imetuahidi. Tuna imani kubwa kwamba Serikali hii inaweza kuyatekeleza mambo mengi tukiwa tumekuwa kama kitu kimoja, na kuwa na ushirikiano katika kuendeleza mambo yetu. Mimi nataka niunge mkono Hoja hii na nashukuru kwa hayo ambayo nimechangia."
}