GET /api/v0.1/hansard/entries/364805/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364805,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364805/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Dukicha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1480,
"legal_name": "Hassan Abdi Dukicha",
"slug": "hassan-abdi-dukicha"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kwa sababu inaangazia suala muhimu sana. Ni kweli kwamba katika nchi hii kuna uhaba mkubwa wa madaktari na madawa. Uhaba wa madaktari umeathiri sana utoaji wa huduma za matibabu kwa jamii, na haswa katika sehemu ninakotoka ya Tana River. Katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni ya Galole, kuna sehemu ambazo ziko umbali wa kilomita 200 kutoka mjini Hola, kama vile Waldena, Wayu, Chifiri na Haroresa. Katika sehemu hizo, kuna uhaba mkubwa wa madaktari na hospitali. Hakuna mabarabara katika maeneo hayo. Kukinyesha, wagonjwa husafirishwa kwa punda mpaka Hola. Hospital ya Hola ndiyo hospitali kubwa pekee katika kaunti, lakini haina vifaa muhimu kama vile chumba cha kuhifadhia maiti na mtambo wa kupigia picha za X-Ray. Madaktari pia ni haba. Madawa na vifaa vingine"
}