GET /api/v0.1/hansard/entries/364808/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 364808,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364808/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "muhimu haviko. Hali ilivyo katika hospitali hiyo ni ya kusikitisha. Hospitali hiyo iko katika hali duni zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, watu wetu hufariki kiholelaholela. Ukiingia kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, utakutana na panya mkubwa zaidi. Sizungumzi utani hapa. Mtu akifariki hapelekwi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Mwili ukipelekwa kwenye chumba hicho, baada ya maasa mawili, paka wanauchukua. Katika jamii ya Waislamu, mtu akifariki huzikwa siku hiyo hiyo. Je, mwili wa Mkristo utahifadhiwaje? Wakristo huhifadhi maiti za watu wao kwa siku kadhaa, hadi mwezi mmoja ama zaidi. Sisi Waislamu, hatupeleki mili ya wafu wetu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo. Mtu akifariki, tunachukua mwili na kwenda kuuzika mara moja kwa sababu tunaogopa. Kwa hivyo, hali katika hospitali hiyo inasikitisha. Mgonjwa akihitaji kupigwa picha ya X-Ray ni lazima aende Garissa ama Malindi, miji ambayo iko umbali wa kilomita 200 na kilomita 250, mtawalia. Kwa hivyo, ni jukumu la Serikali ya Jubilee kuliangazia suala hili muhimu na kuajiri madaktari na wahudumu wa kutosha na kuwapeleka kwenye mahospitali katika kaunti zote nchini. Hivi majuzi, nilikuwa kwenye sherehe ya kumkaribisha nyumbani mhe. Ibrahim Sane wa Garsen. Nilipokuwa nikizungumza na wananchi, niliwaambia kwamba kwa vile watu wetu wengi walifariki kwenye vita vilivyopita, na kulikuwa na amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kwa muda wa takriban mwaka mmoja, basi watu wazae kama sungura. Mwanamke mmoja miongoni mwao akaniuliza: “Sisi hatukatai kuzaa kama sungura. Kwa sababu ya curfew, wanaume siku hizi hurudi nyumbani mapema; tumebahatika. Swali ni kwamba, tutazalia wapi? Tutazalia barabarani kama sungura?” Kusema kweli, hilo ni swali muhimu. Watazalia wapi?"
}