GET /api/v0.1/hansard/entries/364917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 364917,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364917/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kuhusu wafanyikazi wa umma katika sekta ya afya, nikitathmini ya kwamba Wakenya wanaongezeka kwa idadi kubwa sana. Ripoti ya census ya mwaka wa 2009 inaonyesha kwamba Wakenya wanaongezeka kwa kiasi cha milioni moja kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba vifaa vilivyoko kwenye mahospitali yetu haviwezi kukidhi mahitaji ya matibabu ya Wakenya. Kulikuwa na tetezi kwamba ni vizuri wauguzi wetu waende kufanya kazi katika nchi za nje kwa sababu watakuwa wanachangia kuleta fedha za kigeni na kuzisaidia jamii zao. Ningependa kusema kwamba jambo la muhimu ni kuhakikisha kwamba Wakenya wako na afya nzuri, ndiyo wasionekane kuwa watu wanaochangia tu kuongezeka kwa makadirio na matumizi ya Serikali bali pia wanaochangia kukua kwa uchumi."
}