GET /api/v0.1/hansard/entries/364918/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364918,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364918/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia vizuri ni kwa nini nchi za kigeni zinahitaji watabibu wetu na sisi wenyewe hatuwezi kuwaajiri? Ingekuwa ni vyema kama wale ambao tunasema waende kufanya kazi kule nje wangekuwa zaidi ya wale ambao tunaweza kufundisha hapa. Lakini kuwa na mikakati ambayo inaonyesha kwamba vijana wetu wanakwenda shuleni, wanapata masomo ya afya na uuguzi lakini hawawezi kupata kazi, basi ni kuonyesha kwamba tunatumia pesa za umma vibaya. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuhakikisha kwamba kuna utangamano kati ya zile hospitali na zahanati tunatengeneza kutumia zile pesa za umma kama vile CDF na watu watakaoweza kuwahudumia Wakenya kwa ujumla."
}