GET /api/v0.1/hansard/entries/364919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364919,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364919/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Ukiangalia, kwa mfano, ugonjwa wa saratani, umeongezeka kama vile miaka inavyokwenda ilihali, ugonjwa huo unaweza kutibiwa ikiwa kiwango chake hakijaweza kukidhiri. Kwa hivyo, kama hizo zahanati na hospitali zitakuwa na watabibu na wauguzi, itakuwa ni jambo la muhimu kuhakikisha kwamba magonjwa hayo yametibiwa kwa kiwango cha chini. Utakuta kwamba tangu tuanze kuzungumzia maswala ya afya katika Bunge hili la Kumi na Moja, kumekuwa na Miswada minne iliyowasilishwa na Wabunge tofauti kuhusu afya. Tulikuwa na Mswada wa hela za NHIF, wa Emergency Treatment, wa Saratani na sasa huu. Hii inamaanisha kwamba sisi kama nchi tunafaa kufikiria kwa undani na kina na tuwe na motisha kuhakikisha kwamba tuna Mswada ambao utaletwa Bungeni kuhakikisha kwamba kila Mkenya anapata matibabu kwa kiwango kile kinafaa. Kwa sababu, inamaanisha watu wengi, kwa mfano, walio na ulemavu ambao unahitaji kila wakati kupata matibabu, wanaadhirika kwa sababu hospitali ni chache. Utakuta wanatembea kwa muda mrefu kutafuta matibabu ilihali tuna uwezo, nia na njia. Ukiangalia, kwa mfano, yale makadirio ya Bajeti tulipitisha jana, utakuta kwamba Serikali ya kitaifa ina aina nyingi ya matumizi ambayo yanaweza kukatwa kuhakikisha"
}