GET /api/v0.1/hansard/entries/364923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364923/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, nikiunga mkono, ningependa kusema kwamba kama nchi, lazima tuhakikishe kwamba yule Controller wa Budget anaangalia ni mbinu zipi tunatumia katika makadirio ya Serikali kwa sababu nafikiri kuna dosari. Kuna dosari kwa sababu yale mahitaji ya Wakenya, ukikisia vile ambavyo tunatengeneza bajeti yetu--- Umesikia kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ameorodhesha yale mahitaji mengi katika Wizara ya Afya. Umesikia huu Mswada unahitaji pesa nyingi za watu kulipwa ili waajiriwe kuwafanyia Wakenya kazi. Lakini bado utasikia kuna tetesi kwamba hamna pesa. Nikiuliza, ile bajeti ya Serikali ya Kitaifa na ile njia inatumiwa kuhakikisha kwamba tunapata hiyo bajeti haihusishi Wakenya. Ni watu tu wanaketi afisini, wanasema leo wanataka viti vipya, tarakilishi, makaratasi ya kuandikia, kwenda safari nje, kununua maua na utakuta kwamba kiwango kikubwa kinatumika visivyo. Nafikiri ukiangalia, kwa mfano, miaka minne ambayo imepita, tumeongezea bajeti yetu ya kitaifa kutoka Kshs900 bilioni hadi Kshs1.6 trilioni. Itakuwaje kwamba kwa miaka minne peke yake tumeweza kuongeza bajeti yetu kwa zaidi ya asilimia100 ilihali ukiangalia kwa kina, hatutumii hizo fedha kwa yale mahitaji ambayo yatamsaidia mtu wa kiwango cha chini. Utakuta kwamba umaskini umeendelea kukidhiri na ile tofauti ya maskini na matajiri inaendelea kuongezeka. Kwa hivyo, huu Mswada ni wa hali ya juu; ni Mswada ambao unafaa lakini nakisia kwamba hili Bunge letu tunazungumza tu; sijui kuna mikakati gani ya kufuatilia hii Miswada na hata kama inawezekana, tuwe na Mswada hususan wa kuhakikisha kwamba kila Mkenya, awe tajiri ama maskini, anaweza kupata afya kwa kiwango chake na kuhakikisha kwamba ufisadi ambao uko katika mashirika ya afya kama KEMSA, NHIF na mengineo ukomeshwe ili watu wapate matibabu inavyopaswa. Na hizi pesa zikiwekwa katika Wizara ya Afya, zisiwafaidi mabwenyenye wakubwa ambao ni wanabiashara wanaoweza kuingia mle na kusikizana ili hizi pesa zisaidie kuimarisha afya ya Wakenya. Hii ni kwa sababu ikiwa Wakenya watukuwa na afya nzuri, basi itawezekana kwamba sote tutainua kiwango cha uchumi, vijana watapata ajira na tutahakikisha kwamba sio tu kuangalia zile pesa zinatoka nje, lakini Wakenya wakipatiwa nafasi watainua maisha yao kibinafsi."
}