GET /api/v0.1/hansard/entries/364948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364948,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364948/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Kusema ukweli, tuna upungufu mkubwa sana katika nchi hii. Nikiongea hususan katika upande wa Pwani, kuna masikitiko makubwa sana wakati akina mama wanatembea zaidi ya kilomita ishirini kutafuta matibabu. Hata wakifika huko wanapata kwamba huduma ni duni kwa sababu hatuna wauguzi wa kutosha, maabara hayana wasimamizi wa kutosha na hata hakuna vifaa vya kutosha. Bi. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa ieleweke vizuri sana kwamba ijapokuwa tunapigania hao watu waajiriwe ili tupata hiyo huduma, kuna upendeleo katika uajiri. Tarehe nne mwezi wa nne hadi tarehe kumi na sita, watu walikuwa wakisajiriwa ili waweze kupata ajira katika sekta ya afya."
}