GET /api/v0.1/hansard/entries/364995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 364995,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/364995/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Shimbwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1345,
"legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
"slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
},
"content": "Tukiangalia hayo yote, tunaona Katiba ya nchi yetu inatilia mkazo mambo ya afya. Tukiangalia katika historia, nchi yetu ya Kenya iko nyuma katika mambo yote yalioahidiwa wananchi wakati wa Uhuru. Kwa ufupi, tungependelea hata ikiwa hili Bunge linaweza kukubali mambo ya laptop na maziwa ya bure yaondolewe ili tuweze kuhudumia wananchi wetu katika mambo muhimu ya elimu, afya na mishahara ya waalimu, ili tusiwe na mizozo siku za karibuni wananchi, waalimu na madaktari wakiomba mishahara na tushindwe kuwahudumia wananchi wetu. Kwa hivyo, kwa ufupi hata mimi ningeongezea kusema kwamba community health workers wafikiriwe kwa maana wanafanya kazi muhimu katika jamii zetu. Mwisho, kuna mahosipitali ambayo yako kwenye barabara zetu muhimu kama vile Voi na zinginezo. Zingefaa zipatiwe wahudumu wengi kwa sababu ajali nyingi zikitokea kupeleka watu Mombasa ama Nairobi huwa inapoteza wakati mwingi na wengi wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa huduma za haraka."
}