GET /api/v0.1/hansard/entries/365173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365173,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365173/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana mhe. Spika. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ilioko mbele ya Bunge hili letu, kama kijana wa miaka 31 ambaye anajivunia kuwa kijana ambaye anahisi kudhulumiwa. Tumefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba kuna halmashauri ya kitaifa kuhusu vijana, ambayo tulianza kuitetea tangu mwaka wa 2004 na ambayo ilipitishwa miaka minane baadaye; na haijawahi kupatiwa pesa na Serikali tukufu. Mhe. Spika, hili ni jambo la kushangaza kwa sababu ni jana tu Bunge hili liliweza kupitisha makadirio ya Serikali ya mwaka wa 2013/2014. Na hii halmashauri ni mojawapo ya taasisi za Serikali. Mhe. Spika, vijana walirauka na kupigania nafasi za uongozi kutoka mashinani hadi kiwango cha taifa wakati wa uchaguzi wa halmashauri hii. Uchaguzi ulipoitishwa na Waziri aliyekuwemo, kulikuwa na tetezi kubwa sana; kulikuwa na makabiliano."
}