GET /api/v0.1/hansard/entries/365174/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365174,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365174/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Kuwapatia vijana nafasi ilikuwa ni njia moja ya kuwahusisha katika siasa lakini wakaonekana kama watu mboga uongozini. Lakini siyo hivyo. Hii halmashauri ya Kitaifa ya Vijana ni kama ile Maendeleo ya Wanawake. Inawapa vijana wasia mwafaka kujionyesha kwamba wao wana demokrasia na wanaweza kuwa na viongozi ambao watazungumza kwa niaba yao kwa sababu wamechaguliwa na vijana kama wao. Bw. Spika, kipengele cha nne cha sheria ambayo imetengeneza hili baraza imesema kinaga ubaga yale mambo ambayo litafanya. Kwa mfano, inasema kwamba baraza hili litakuwa likihusika katika kushirikisha miradi na mikakati ya kitaifa kwa vijana. Hili ni jambo muhimu kwa sababu watu wengi wamekuwa wakijaribu kuwasaidia vijana wetu, lakini hata Serikali haijui ni nani anayefanya lipi na wapi. Kwa hivyo, baraza hili litaweza kuwa na orodha ya miradi na mikakati na hata fedha ambazo zimetengewa vijana ndio tuwe na uiano kwamba tunaweza kuwasaidia vijana kama taifa."
}