GET /api/v0.1/hansard/entries/365180/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365180,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365180/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kama hili baraza litapatiwa nguvu, litaongeza sauti ya vijana katika mashirika ya maamuzi ya umma. Pia, itakuwa sauti nzito ambaye itasikika kuhakikisha kwamba asilimia sabini na tano ya wakenya ambao wako chini ya miaka 35 wanahusishwa katika shughuli za nchi hii. Ni muhimu kufanya vile kwa sababu kama vile takwimu zinaonyesha, kufikia mwaka wa 2017, kutakuwa na vijana zaidi ya milioni 24 ambao watakuwa chini ya miaka 35. Kama hatutaangazia sana maswala ya vijana, basi ni kama tutakuwa tumekalia bomu la muda. Ningependa kuhimiza Serikali ya Jubilee ambayo imechaguliwa kwa kusema sana kuhusu vijana na akina mama, kwamba inafaa kuchukua nafasi hii kuhakikisha kwamba baraza hili la vijana limepewa nguvu. Wanafaa kufuatilia maneno yao na vitendo. Wametuambia “ I believe kusema na kutenda”. Basi tunawaambia kwamba waseme na watende na wawapatie vijana nafasi. Hili litakuwa jambo la muhimu kwa sababu, kwa mfano, hatujaona Waziri au Katibu ambaye ni kijana. Kwa hivyo, kulipatia baraza hili fedha kutakuwa ni kupigia upato na kuonyesha kwamba kuna kujitolea kwa Serikali kuhakikisha kwamba vijana wana nafasi. Hili baraza pia lina nafasi ya kuhakikisha kwamba Hazina ya Biashara ya Vijana imeimarishwa, kusawazishwa na kufikisha hela mashinani. Kwa hivyo, hatuwezi kusema kuwa hili baraza halina kazi au ni la kisiasa. Hatuwezi tukasema kwamba hili baraza ni la vijana ambao tu ni kama msala upitao"
}