GET /api/v0.1/hansard/entries/365198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365198,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365198/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii inayohusu vijana. Hii ni kwa sababu tukiweza kutimiza yale yaliyo katika hii Hoja tutakuwa tumewasaidia vijana wetu kwa vile wametufanyia kazi nzuri. Wakati wa kura za 2007 tuliambiwa kwamba vijana walifanya fujo. Tulirudi mashinani tukaongea nao. Wakati huu tulipiga kura na hapakutokea fujo yoyote. Hii itakuwa ni zawadi kubwa sana kwa watoto wetu. Hii Hoja itawarekebisha vijana kinyume na wanavyofikiria wengi. Wabunge wenzangu, huko Kwale vijana wangu walisema kwamba Wabunge wapewe pesa. Hii ni kwa sababu kila uchao vijana wako mlangoni. Asubuhi ukiamka unapata SMS zaidi ya 1000 kwenye simu, “Twataka kazi.” Tukipitisha hii Hoja, nafikiri hizo SMS hazitaonekana tena katika simu zetu. Wakati ilipotangazwa kwamba pesa za vijana zimetolewa ama kwa kweli zile pesa hazikuwa zimemlenga kijana. Zilikuwa zimelenga wengine wajitajirishe. Kwa nini hizi pesa zilipelekwa kwenye mabenki na hali wanajua wazi kwamba hakuna kijana Mkenya ambaye ana security ? Kijana hana title deed . Shamba ni la babake ama ndugu zake. Hizo pesa zimetajirisha wengine na vijana wetu wamebakia mtaani. Naiomba hii Serikali kupitia Rais Uhuru ambaye pia ni kijana ijitolee mhanga ili wazitoe zile pesa kutoka kwenye mikono ya mabwanyenye. Wafanye vile vile pesa za akina mama. Hizo pesa ziwekwe kwenye mikono ya Wabunge wa majimbo. Huyu mama ataweza kulinda wanawake kwa sababu anajua kugawa. Hawezi kumaliza chakula kwenye chungu; hubakisha akamwekea mwanawe. Hizo pesa zikiwa katika mikono yetu vijana wataweza kufanya miradi yao na tutakuwa pale kumwonyesha njia."
}