GET /api/v0.1/hansard/entries/365318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365318/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama hapa kuunga mkono Hoja hii ambayo inazungumzia swala la baraza la vijana. Kwa hakika, ni masikitiko makubwa kuona katika nchi yetu mpaka sasa hivi, baada ya kuwa tumelipitisha baraza hili, hatujalipatia ufadhili wa kuweza kufanya utendaji kazi. Tunajua vijana katika nchi hii yetu Kenya ni zaidi ya asilimia 70. Hivyo basi, wao ndio wengi katika asilimia ya wakenya wote. Ni masikitiko kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yamechukua kipao mbele kuunganisha vijana kuliko sisi wenyewe ambao ndio tunatawala nchi yetu ya Kenya. Kwa mfano, kuna mashirika kama Youth Agenda ama Youth Assembly. Hayo yote ni mashirika ambayo yanapata ufadhili kwa mashirika yasio ya kiserikali. Yafaa sisi wakenya tuchukue jukumu la kuangalia vijana wetu. Kwanza kabisa, wakati tunapata baraza hili, ni sawa na kupata sauti ya vijana. Kupata sauti ya vijana, haitakuwa sauti, ikiwa haitakuwa na hazina ama fedha za kuwawezesha kutatua matatizo yao na changamoto zao ambazo zinawakumba katika maisha yao. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunajua ile hazina ya pesa za vijana ambayo kwa Kiingereza ni Youth Enterprise Development Fund. Fedha hizi zimekumbwa na changamoto nyingi kwa sababu wakati vijana wanapewa pesa hizo kupitia mikopo, wanatumia vibaya. Pia, kwa sababu hawana mbinu nzuri za kutumia vizuri katika upande wa biashara; hivyo basi pesa hizo hazirudi. Pesa hizi ni pesa ambazo zinatumiwa kwa njia ya mviringo; yaani kwa Kiingereza, revolving fund. Pesa ambazo utachukua na urejeshe na pia vijana wengine waweze kuzichukua. Mhe. Naibu Spika wa Muda, baraza hilo likiwa limepatiwa fedha na kuweza kujimudu, litaweza kuwafuatilia vijana hao ama vikundi vya vijana ambao wanachukua pesa kama hizo na kuweza kusaidia Serikali yetu katika mpango kama huo. Vile vile, tunajua hivi sasa hakuna Wizara ambayo inasimamia mambo kuhusu jinsia, watoto na hata vijana. Hivyo basi, Wizara kama ya michezo ikiweza kushirikiana na baraza kama hili, itaweza kutafuta vijana ambao wana talanta. Hivi sasa tuna vijana ambao wameingia katika michezo sana, kuna kama dada zetu kama Wahu Mathenge, Jua Kali, Fisherman na kadhalika. Hawa ni vijana wametoboa katika mambo ya uimbaji. Lakini masikitiko ni kwamba, uimbaji wao ama talanta hizo zinapotea bure na wala haziwafaidi. Hayo yote ni kwa sababu hawana chombo cha kuzungumzia. Changamoto zao ni kwamba hawana chombo cha kuweza kuwanyongoa uwezo katika talanta hizo wanazo. Mhe. Bi. Naibu Spika wa Muda, pia vijana wana changamoto katika dawa za kulevya, mvinyo, na pia sasa hivi tunaona vijana wanatumiwa katika ngono zisizo halali kama vile matukio ya juzi katika upande wa Mombasa ambapo dada zetu, ambao ni"
}