GET /api/v0.1/hansard/entries/365321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365321,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365321/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "vijana, walitumika katika mambo kama hayo mabaya. Mpaka sasa, hakuna chombo chochote cha vijana ama baraza lolote la vijana ambalo limezimama kidete na kusema: Ijapokuwa watu hawa walikuwa ni watalii wanaokuja nchi, yetu, wametenda jambo ambalo si la halali. Hayo yote ni kwamba, tulikosa kutowajumuisha na kuwapatia mwelekeo. Kwa vijana kuongoka ama kuendelea, lazima wapate mwongozo. Mhe. Bi. Naibu Spika wa Muda, tunataka kazi kwa vijana. Hapo awali tulikuwa na kazi kwa vijana ambayo ilikuwa ni kazi ya ajira ya siku kadhaa ama kibarua. Sasa hivi, tunapolipatia uwezo baraza la vijana, tutaweza kuja na ajira gani ambazo zitakuwa za kupitia kandarasi? Vijana wapewe kandarasi ya miaka miwili, mitatu au mitano. Pia, vijana waweze kutengeneza kampuni ili waweze kutengeza sabuni kupitia Serikali yetu ambayo inatoa sabuni nyingi kila wakati kuweza kuwaboresha na kujenga ajira kwa vijana wetu. Kenya ni nchi ambayo hivi sasa haitataka kutumia vijana wakati tumeshikwa na dharura ama wakati wa majanga. Kwa mfano, tukisikia kumekuwa na shida ya Mombasa Republic Council (MRC); tukisikia kuna shida ya Al Shabaab, ndio tunakumbuka vijana, Lazima tulipatie hazina baraza hili ili liwe lina mikakati ya kuweza kuwafunza hawa vijana na kuwabadilisha mawazo yao. Wawe ni vijana ambao wanajua ni Kenya kwanza na wao ni wa pili. Bila ya kufanya hivyo, ikiwa tutakuwa tu ni wakati wa majanga basi siku zote vijana watabadilisha mawazo na watakuwa MRC, Al Shabaab na watakuwa katika matukio hayo yote. Sisi ndio wa kwanza kusema vijana wanatumiwa vibaya."
}