GET /api/v0.1/hansard/entries/365723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 365723,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365723/?format=api",
"text_counter": 18,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Naibu Spika wa Muda, namshukuru Mhe. Mburu kwa kunikabidhi fursa hii ili nichangie Hoja hii ambayo ni ya muhimu kwetu. Uchumi wa nchi yetu, asilimia 90 unategemea mawasiliano na uchukuzi wa barabara. Sote tunajua kwamba baadhi ya sababu ambazo zinachangia kuzoroteka kwa barabara hasa ni wakati wa mvua. Sehemu ambayo ninawakilisha ya Saboti, inakisiwa kuwa na watu karibu 200,000. Lakini hakuna barabara yoyote maalum ambayo tunaweza kuita highway. Watu wa Saboti wanajulikana - na watu wa Trans Nzoia kwa ujumla - kuwa wakulima. Lakini tukienda upande wa barabara, kama ni namba, labda tupewe kuanzia mwisho katika sehemu ambazo hazina barabara nzuri. Wakulima kutoka Trans Nzoia wameumia sana na pia wanakosa huduma muhimu kwa sababu ya barabara mbovu wakati mvua inanyesha. Najua kwamba hii Hoja ikizingatiwa, nchi yetu itanufaika sana. Ahsante!"
}