GET /api/v0.1/hansard/entries/365767/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 365767,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365767/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa mhe. Zuleikha kwa kunipa dakika mbili za muda wake ili niweze kuchangia Hoja hii. Ningependa kusema kwamba Hoja hii ni nzuri kwa sababu katika taifa letu la Kenya, tumeona mara nyingi masuala ya vijana, ambayo ni muhimu sana kwa taifa hili, yakiwekwa nyuma. Kwa hivyo, ningependa kuiunga mkono Hoja hii kwa dhati kwa sababu ninafahamu kwamba iwapo vijana watapata fedha, watapata nafasi ya kujiendeleza na kuleta maendeleo katika taifa hili. Ni kweli kwamba suala la kusema vijana ni viongozi wa kesho limepitwa na wakati. Naamini kwamba tukitoa fedha kwa vijana na wapewe nafasi ya kuzitumia vizuri, fedha hizo zitaendeleza mipango ya vijana humu nchini. Hatutaki kusikia tena vijana wakijiingiza kwenye shida za mihadarati ama wakiwekwa katika ngazi ya chini. Mara nyingi, vijana huchukuliwa kuwa watu wa kuendesha pikipiki za boda boda, kufanya kazi duni na kutumiwa vibaya, haswa wakati wa kampeini za kisiasa. Sheria inasema kwamba ni lazima pesa hizo zitolewe kwa vijana ili vijana waweze kuendeleza miradi yao ndiyo tuweze kupata maendeleo katika nchi hii."
}