GET /api/v0.1/hansard/entries/365909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 365909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/365909/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii kuhusu mtoto wa kike. Sisi tunaoishi katika sehemu kame sio kwamba tuliomba kuishi kule bali ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Serikali zilizopita zilitutenga ndio maana tumeamua kuwa na Hoja kama hii. Namuunga mkono Mhe. Dukicha kwa kuleta Hoja hii. Kwa kweli hakuna shule katika sehemu kame. Hata kama mtazungumzia CDF, tunafahamu kwamba imekuja juzi tu. Miaka ya nyuma shule hazikujengwa. Kuna sehemu za wafugaji wanaotafutia wanyama wao lishe. Wao hata hawana nafasi ya kusoma. Ndiposa tunaonelea kuwe na shule ambako watoto watalala na kusoma. Mimi nazungumzia watoto wote wa kike na wa kiume wanaoishi katika sehemu hizi kame. Mwenzangu amesema kuwa nchi nzima inafaa kuangaliwa kupitia Hoja hii. Lakini kuna kule ambako ni Kenya na kule ambako ni Kenya nusu. Kwa hivyo, Kenya nusu nayo ivutwe angalau ifike karibu na Kenya nzima ndio tujihesabu kuwa katika nchi moja. Hii haitafanyika mpaka mambo ya elimu yaangiliwe na yatekelezwe kwa wakati unaofaa. Kwa sababu ya ukosefu wa elimu katika maeneo kame, ile hesabu inapoletwa kwamba watu waajiriwe kwa kiwango fulani, sisi tunakosa hizo nafasi. Kwa upande wa kuwaajiri askari au wauguzi, tunakosa nafasi. Tunaletewa watu kule kwetu ambao hawako tayari kufanya kazi kule. Mtu anaajiriwa kazi leo na baada ya miezi mitatu anaomba kuhamishwa. Anasema huko kuna shida nyingi. Kwa hivyo, tupewe hizi nafasi. Serikali inafaa kutoa pesa za kutosha na kutujengea mashule ili watoto hawa wasome na kuwa watu ambao watatuhudumia kule kwetu, ambako wengine hawataki kufanya kazi. Kama alivyosema mhe. Shaban, wengine wanapatiwa pesa za kuwsaidia katika sehemu ambazo zina uzito wa utendaji wa kazi, lakini hawastahili kupewa hizo pesa na"
}