GET /api/v0.1/hansard/entries/368559/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 368559,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/368559/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Katika Hotuba ya kwanza ya Rais wa Taifa hili, Baba wa Taifa Mzee Jomo Kenyatta alitoa changamoto tatu kubwa ambazo ni umaskini, kutojua kusoma na kuandika na maradhi. Ni kwa nini kutoka miaka 50 iliyopita mpaka leo hatujapata zuluhisho la matatizo haya? Tunapozungumzia kuhusu elimu ya watoto, elimu ya watoto wanaoishi katika sehemu kame ni nadharia. Ikiwa watoto wa Kenya wana matatizo, watoto wa kutoka sehemu kame ya Kenya au watoto wa wafugaji wana matatizo mara kumi ukilinganisha na watoto wale wengine. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu watoto wa wafugaji ni watoto ambao wanategemea mazingara. Ikiwa kumenyesha na kuna nyasi ya kutosha, wanapata fursa ya kusoma. Kukiwa na ukame, inabidi watoto hao watoke wanapoishi ili watafute malisho ya mifugo. Watoto hao wanaathirika."
}