GET /api/v0.1/hansard/entries/369367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 369367,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/369367/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Kwa hivyo, shirika hili likibuniwa nafikiri litakuwa ni jambo muhimu sana. Niseme kwamba Hoja hii ingepingwa na wale ambao kila baada ya muda hutaka kujinufaisha kutokana na majanga ya watu. Ni vizuri pia tuwe na hili shirika kwa sababu Wakenya wenyewe hawajaweza kuhamasishwa ni vipi ambavyo wanaweza kujikinga na adhari za majanga ambayo yanatokea. Kwa mfano, hata ukiangalia nyumba, wanawezaje kujikinga na moto ukitokea? Kwa hivyo, nimesimama kuunga mkono. Natumaini kwamba hii Hoja inaweza kuhakikisha kupunguka kwa nafasi ya watu ambao hufaidika kutokana na shida za watu wengine."
}