GET /api/v0.1/hansard/entries/369422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 369422,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/369422/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mafuriko pia huharibu mimea. Watu wanatayarisha mashamba yao na mimea inaanza kumea. Lakini mafuriko yanachukua kila kitu na watu wanabaki hohehahe. Vile vile, mafuriko huleta ugonjwa wa kipindupindu katika sehemu kame na watu huadhirika sana kwa sababu hakuna madawa hospitalini. Jambo hilo linaleta tashwishi nyingi sana. Mafuriko pia huadhiri mifugo kwa sababu hawawezi kwenda marishoni. Kwa hivyo, ni jukumu la Serikali ya Jubilee kuhakikisha kwamba shirika hili limeundwa ili majukumu haya muhimu yatekelezwe. Naunga mkono."
}