GET /api/v0.1/hansard/entries/369927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 369927,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/369927/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Nina matatizo kidogo; ni kama nimepoteza kadi yangu na haijulikani iko wapi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ina maana kwa Wakenya. Lakini mbona tunangoja mpaka wakati matatizo yanatokea ndio watu waende mbio? Mambo ya mafuriko yamekuwa ni kama kitega uchumi kwa wengine. Wakati mafuriko yanatokea, utaona bajeti kubwa kubwa zinazinduliwa kutoka mahali ambapo hapaeleweki na hizo pesa zitatumika na watu hawaelewi zinatumika vipi. Hizo pesa zinazotumika wakati wa mafuriko hazingetumika kama tungekuwa na mipangilio ya maana. Hayo mafuriko hayangeweza kutusumbua tena katika Kenya hii. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kuna sehemu ambazo zinajulikana wazi kwamba lazima mafuriko yazikumbe kila mwaka. Ni kwa sababu gani Serikali haijachukua hatua ya kuwa na msimamo ama mpangilio maalumu kama vile wa kutengeneza mabawa ambayo yatachukua maji wakati wa mvua? Serikali inaweza kuwahamisha wale wananchi wanaoathirika na kuwapatia makao katika sehemu ambazo wataweza kuishi bila kuathirika na mafuriko yanapotokea. Mhe. Naibu Spika wa Muda, pia yafaa tuwe na watu ambao wako na mafunzo maalumu ya kuweza kutokea mara moja na kuokoa maisha ya watu wakati mafuriko yanatokea. Hili neno litakuwa ni hadithi ambazo zitakuwa zikiendelea kila siku kama mjadala na watu watakuwa wanakufa. Pesa zitakuwa zikitumika kwa njia ambazo si nzuri, na hakuna chochote kitapatikana kwa manufaa ya Wakenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ijapokuwa tutaunga mkono Hoja hii, lakini wakati umefika tuwe na chombo ama taasisi ambayo itaweza kusimamia mambo ya mafuriko na sio mafuriko tu, lakini pia ajali yoyote ambayo inaweza kuleta maafa makubwa katika nchi hii."
}