GET /api/v0.1/hansard/entries/371136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 371136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/371136/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga)",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ikiwa kweli Serikali ya Jubilee imeamua kupambana na ufisadi, tunataka tuanze kuyaona hayo mapambano kuanzia waliokuwa na mamlaka. Waregeshe mali ya Wakenya. Wale waliokuwa na mamlaka watuonyeshe mfano mzuri kabla hawajapelekwa kortini kwa kujitokeza. Naomba kile kiboko ambacho Jubilee inatumia, ikitumie ili waliochukua pesa zetu na kuzipeleka katika nchi za nje, waadhibiwe. Goldenberg inafaa kufufuliwa upya ili haki itendeke kwa Wakenya. Tukifanya hivyo, hakuna mwingine atakayedhubutu kufanya ufisadi kwa sababu atakuwa anajua mkono wa sheria unafanya kazi."
}