GET /api/v0.1/hansard/entries/371436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 371436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/371436/?format=api",
    "text_counter": 501,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa na rafiki yangu, mhe. Bowen Kangongo. Ikiwa tunataka kuwa na nchi ambayo ina viwanda na inanawiri katika uchumi, ni lazima tuhakikishe kwamba watu wanapata stima ili wafanye miradi yao vizuri. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni jambo la kushangaza kuona kwamba ni asilimia 15 ya Wakenya ambao wana umeme. Hili linaweza kushangaza wengi kwa sababu ukiangalia, unaweza kufikiri ni watu wengi sana ambao wamesambaziwa umeme, wale ambao wamekaribia mitaa na miji mikubwa kama vile Nairobi, Kisumu, Nakuru, na kadhalika. Lakini kwa sababu ya"
}