GET /api/v0.1/hansard/entries/371439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 371439,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/371439/?format=api",
"text_counter": 504,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "umeme, watu wengi wanakimbilia mijini ili waweze kujitafutia riziki yao ya kila siku. Lazima tuhakikishe kwamba huduma za jamii na za umma zinakwenda mashinani. Ni muhimu kuhakikisha kwamba umeme umegatuliwa pia, ili watu waweze kupata nafasi ya ajira. Zile zana ambazo wako nazo za kujiendeleza ziweze kupata mwanya wa kuafikiwa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ikiwa kijana mdogo ana ndoto ya kuweza kufanya ukarabati ili awe na taaluma fulani, lazima kuwe na vifaa. Vifaa vingi vya kumwezesha kuendeleza hiyo taaluma yake hutumia umeme. Kwa hivyo, hili ni jambo muhimu sana. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kule Uropa utakuta karibu bara nzima lina stima na watu wengi wana mataa kwao nyumbani. Barabara zinaonekana ukiwa angaani. Lakini ukitoka safarini Afrika Kusini kuja Kenya, isipokuwa tu uone mwangaza kule Johannesburg na Durban, kule kwengine ni giza totoro. Kwa hivyo, hilo ni jambo ambalo linaonyesha kwamba kwa kweli, Afrika kama Bara bado liko gizani. Pale ambapo pana mwangaza pia pana usalama. Kuna Wabunge kadhaa ambao wameweka stima, kwa Kiingereza flood lights kule sokoni. Kufanya hivyo kumewawezesha akina mama kufanya kazi zao. Kuna ambao wanakwenda sokoni hata baada ya usiku kuingia. Kwa hivyo, uzuri wa umeme ni kutuwezesha kama nchi kuwa na usalama."
}