GET /api/v0.1/hansard/entries/372254/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 372254,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/372254/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Ashante sana, Mhe. Bowen kwa fursa hii. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni Hoja ambayo imekuwa mara kwa mara katika Serikali ya Kenya, tukiangalia Shirika la Kenya Power likiwa na uzembe wa kupeleka huduma zao kwa wananchi. Kulingana na mfumo wa kibiashara, lazima kuwe na mashindano. Yakiwemo mashindano, nina hakika yale malipo ambayo wananchi wanatakikana kulipa yatashuka. Mwezi huu wa Ramadhani, sisi Waislamu tunatumia wakati wa usiku kupeleka maombi yetu, kukaa vizuri na kuomba Mungu ili atusamehe makosa na dhambi zetu. Kwa hivyo, ninaomba Kenya Power wapunguze visa vya kukata stima wakati wa usiku kwa sababu tuko katika harakati za kuomba Mungu wetu wakati huu wa mwezi wa Ramadhani. Vile vile, tukiwa Vanga, tunatumia stima kutoka Tanzania. Sasa hivi, Tanzania pia wanatukatia stima. Sisi Wakenya tuko katika mpaka wa Kenya na Tanzania. Shirika la Kenya Power limeshindwa kufikisha stima kwetu ndio sababu tunatumia stima kutoka Tanzania. Kwa hivyo, tunaomba shirika la Kenya Power lihakikishe kupitia kwa Rural Electrification Authority (REA) kwamba tunapata umeme. Kwa sababu ya huu mradi wa Serikali unaokuja, naona kila mahali stima itasambazwa, itapenya katika shule. Kwa hivyo, ninaomba kwamba REA ambao wanafanya kazi nzuri, wahakikishe kwamba stima inafika katika maeneo wananchi wanamoishi. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii na kumshukuru mhe. Bowen."
}