GET /api/v0.1/hansard/entries/372747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 372747,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/372747/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Chuo Kikuu cha Nairobi alituachia wasia kwamba tukiingia siasa basi tufanye siasa ya utu na heshima. Bahati yangu ilikuwa kwamba baba yangu alikuwa kiongozi katika Bunge hili na alifanya kazi pamaja na mama Chelagat na hata wewe Mhe. Spika. Siku moja nilimwuliza mzee, “Je, hawa viongozi walioko Opposition mnazungumza nao namna gani?” Wakati huo nilikuwa namzungumzia mhe. Anyona. Baba yangu alisema hivi: “Hawa viongozi unavyowaona kuna mambo mazito ambayo wangependa kushughulikia ambayo wananchi wengi hawafikirii vilivyo kwa sababu wanaona ile kelele ya siasa ya upinzani”. Ningependa kuwasihi wenzangu kwamba ikiwezekana tuanze kuwaenzi sasa viongozi kama Chelagat Mutai kwa kuwataja katika shule zetu. Kwa mfano, ningependa kuita shule moja katika eneo Bunge la Kitutu Chache, “Chelagat Mutai High School”."
}