GET /api/v0.1/hansard/entries/372881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 372881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/372881/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Mhe. Spika, mimi ni mwanachama wa Kamati ya Uchukuzi na Ujenzi na Makazi. Jana tulikuwa na kikao na Waziri anayehusika na masuala hayo. Kilichoibukwa kwenye kikao hicho ni kwamba hakuna sheria inayomuruhusu kuchukua pesa za barabara na kuzipeleka kwa serekiali za kaunti. Kwa hivyo, kama Kamati, tuliketi na kulizungumzia jambo hilo. Waziri aliomba muda. Kufikia Jumatatu ijayo, ataleta jawabu lakini hakikisho ni kwamba ni kinyume cha sheria kupeleka pesa za barabara kwa magavana, mpaka Bunge litakapobatilisha sheria iliyopo. Sheria ya Roads Levy Fund bado inatumika. Hadi sheria hiyo itakapobatilishwa, ni lazima pesa za barabara ziende kwa maeneo Bunge. Ahsante, mhe. Spika."
}